Upendo Benson



Nasikia kuchemka ndani yangu... uuh! Sikia usimtendee mtu mema eti kwasababu alishawahi kukutendea mema, usionyeshe upendo kwa mtu kwasababu tu na yeye anaonyesha upendo kwako, usisaidie mtu kwasababu alishawahi kukusaidia au unategemea siku moja na wewe ukiwa na shida atakuja kukusadia... kwa kufanya hivyo hakuna tofauti yoyote, maana hata wana wa dunia hii hufanya hivyo hivyo... Sisi tumeshabadilishwa nia zetu na kuwa kama Kristo, hatufanyi tena kwa namna ya dunia hii.. maana hata Baba yetu wa mbinguni huwanyeshea mvua waovu na wema(Matt 5:45).. huwa habagui aah! Tunatakiwa kutenda mema wakati wote bila kuangalia upande wa pili walishatutendea mema au la, tuwe na upendo.. tuwapende adui zetu na kuwaombea wanaotuudhi(Matt 5:44).. tusaidie hata wale ambao hawatusaidii, na tunaposaidia tusitegemee kupokea kitu kutoka kwao bali katika yote hayo tunafanya kwasababu ndio asili yetu.. nakuhakikishia kwa kufanya hivyo utayafurahia maisha, maana utakuwa huru bila mizigo ya kubeba watu rohoni mwako. #Badonajifunza

Nina mambo mawiliya kukuambia

1. Wakati mwingine unaweza usijue una uwezo kiasi gani katika hicho unachofanya mpaka umekaa chini na kujifunza kutoka kwa wanaojua/waalimu.. coz unaweza jiona unajua kumbe hujui.. na hiyo ikasababisha ukafanya mambo yasiyokuwa na ubora.

2. Mtu yeyote anaweza kutumiwa na shetani kwa lengo la kukukwaza, kukukasirisha au kukufanya ukose amani ambayo inaweza kukupelekea kujenga chuki/uadui ndani yako ukamkosea Mungu bure, lakini ukiwa mjanja unaweza kutumia hayo makwazo kama moja ya somo la vitendo kukupa uzoefu katika kusamehe.
(Jifunze kujifunza, ufurahie maisha)

MWALIKO

Hallow,

kama unaamini unakipaji cha utunzi wa simulizi. Wasiliana nasi uweze kupata nafasi ya kuweka hadithi zako humu.

Faida utakayopata

utapata wasomaji wengi kimataifa
utapata wadhamini
utaweza kuhifadhi kumbukumbu za hadithi zako humu kwa muda mrefu.

KARIBU

David J Mangare

manager