Chief Nemes




UTARITHISHWA, UTARITHI, UTARITHISHA
Story by; Nemes Mnyanga (Chief)
                                                                 Nemes akiwa amemshika Gamba

   Iliikua alfajiri huku jua la asubuhi likiwa linachomoza na upepo mzuri ukipuliza miti iliyozunguka shamba hilo, na sauti za vyura pamoja na ndege wakiipamba kwa sauti zao maridadi asubuhi ile.

   Ndipo mvulana shupavu na jasiri aliyejengeka vyema mwili kutokana na kazi ngumu ya kukata magogo ya miti na kuyabeba, Kijana huyo aitwae Nemes Mnyanga alipoonekana akitua shoka na jembe chini, kisha akatoa fulana kuu kuu aliyokua amevaa akiacha kifua chake kionekane vyema....

   Na hizi shughuli za kukata mkaa ndizo zilizofanya kijiji chote cha Mandela kimjue na kumpenda kwa ushupavu wake.

Kama ilivyo siku zote aendazo kukata magogo, lakini siku hii ilikua tofauti. Wakati anashusha shoka la kwanza kuelekea kukata mti mkubwa uliokwisha kukauka, akasikia kwa ukaribu takribani kilomita chache, mwanaume akipiga kelele za kuomba msaada toka shambani, kelele zilipozidi, akatupa jembe na kuchukua shoka lake kama silaha tayari kuelekea kelele zinapotokea kukabiliana na hatari anayoweza kukutana nayo.

JE UKO SHAMBANI KIMETOEA NINI?

Akiwa mwenye hamaki na jasho jingi likimtoka japo ilikua ni alfajiri na kuna ubaridi mkali, lakini kwake ilikua tofauti, alikuwa akipiga mbio huku mkono wa kulia ameshika shoka lake na mkono wa kushoto anautumia kuachanisha miti na majani yalisonga njia japo miba ni mingi hakujali, alichojali ni kumfikia mwanaume huyo ambaye alikuwa akiendelea kupiga mayowe yenye uchungu mkali na yakiashiria anakata tamaa ya kupata msaada, lakini cha kushangaza, alipokua anakaribia maeneo ya sauti inapotokea akagundua My God! hii si sauti ya GAMBA..!! Nemes alisikika akishitushwa zaidi na wasiwasi ukimzidi. Kijana Gamba alikuwa anajishughulisha na kilimo cha mpunga kwa miaka yote. Ndipo Nemes anavuta pumzi na kuongeza spidi kutokomea katika shamba la mpunga la kijana Gamba. Hatua chache mbele yake anaona kimbunga kikubwa kilichokusanya vumbi na majani, kikimuelekea rafiki yake aliyekua chini akijisogeza kukikimbia kimbunga kile, akionyesha tayari amekwisha ishiwa nguvu na miguu yake ikiwa na hali ya ganzi,

Wakati Nemes amesimama akitetemeka angali jasho likimmiminika, akiwa anafikiria atawezaje kumwokoa rafiki yake, tayari kimbunga kipo karibu nae, hana la kufanya. Alisikika akiita,
Gambaaaaaa….! Nooooo..! Noooo..!
kimbunga kilienda na kumzoa Gamba kikamkusanya na kumtupa bila huruma katika tope zito pembeni ya shamba lake kasha kikapotea.
Huku Nemes akiwa anakuja mbio akiendelea kuita na machozi na jasho jingi vikimtoka hakuwa akiamini kinachotokea mbele yake, akitamani ingekuwa ni ndoto, kwani upendo wake kwa rafiki yake ulikuwa hauna unafki.
Anafika mpaka alipo anguka Gamba na kumuinua upande wa shingo uku akimuuliza kilichomtokea Gamba,
“Gamba Ga...Gambaaa tafadhali nieleze nini kimetokea…”
lakini Gamba mwenye maumivu makali akihema kwa tabu sana na akiwa amejawa na udongo mwilini mwake mithili ya mtu aliyefukuliwa chini ya ardhi alikua awezi kusema zaidi ya kuonyesha jeraha kubwa lililokua likivuja damu katika mguu wake wa kushoto.
Kutokana na ujasiri wa nemes anafikiri kwa haraka na kumbeba Gamba tayari kuelekea kijijini,
Nemes anamuinua Gamba anamtia begani bila kusahau shoka lake, anaanza kukimbia kuelekea kijijini huku rafiki yake akiwa begani akilia kwa uchungu….,

Jee nini kimemtokea Gamba akiwa shamban na jee itakuaje safari ya nemes kumrudisha gamba kijijini??

Usikose episode ya pili ya simulizi hii yenye kusisimua.

2 comments:

MWALIKO

Hallow,

kama unaamini unakipaji cha utunzi wa simulizi. Wasiliana nasi uweze kupata nafasi ya kuweka hadithi zako humu.

Faida utakayopata

utapata wasomaji wengi kimataifa
utapata wadhamini
utaweza kuhifadhi kumbukumbu za hadithi zako humu kwa muda mrefu.

KARIBU

David J Mangare

manager